Ajira
Ili kutimiza majukumu ya Shirika tunahitaji wataalamu wenye ubunifu na utayari kufanya kazi ili kwenda mbele zaidi kwa ajili ya manufaa yao, wateja na Shirika. Ukiwa nasi utaweza kutimiza malengo yako na ujuzi wa kitaalam kwa kupata nafasi ya kufanya kazi nasi na kupata ujuzi kupitia mafunzo mbalimbali ambayo yataongeza ujuzi na kukujenga kimaarifa. Tunaamini kwamba hatua tunayopiga pamoja inaweza kutupeleka mbali zaidi.
Shirika la Reli Tanzania linatoa nafasi mbalimbali, kama upo tayari kufanya kazi nasi kwenye maeneo haya; Huduma za kisheria,Huduma, Biashara, Ulinzi na Usalama, Ukaguzi wa Ndani, Fedha, Mahusiano, Mipango na Hudma za Kiutawala, Usafirishaji Mawasiliano ya Simu, Uhandisi Mitambo, Uhandisi Ujenzi, Rasilimali Watu, Manunuzi na Ugavi na Afya.
Nafasi yoyote ya kazi itakayotokea ndani ya Shirika la Reli Tanzania itatangazwa kwenye tovuti hii kwa lengo la kuutaarifu umma. Kwenye orodha ni baadhi ya fani ambazo unaweza kuzipata endapo utapenda kufanya kazi na Shirika la Reli Tanzania;
- Huduma za kisheria
- Huduma ya Teknolojia ya Habari
- Biashara
- Ulinzi na Usalama
- Ukaguzi wa Ndani
- Fedha
- Mahusiano
- Mipango na Hudma za Kiutawala
- Usafirishaji
- Mawasiliano ya Simu
- Uhandisi Mitambo
- Uhandisi Ujenzi
- Rasilimali Watu
- Manunuzi na Ugavi
- Afya