Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

KUONGEZEKA KWA SIKU ZA SAFARI ZA TRENI YA ABIRIA DAR ES SALAAM – KILIMANJARO24
December
2019

SHIRIKA LA RELI TANZANIA - TRC LINAWATANGAZIA WATEJA WANAOTUMIA HUDUMA YA USAFIRI WA RELI NCHINI, KUONGEZEKA KWA IDADI YA SIKU ZA SAFARI KWA TRENI YA ABIRIA KUTOKA DAR ES SALAAM KUELEKEA MOSHI MKOANI KILIMANJARO, KUTOKANA NA MAOMBI YA UHITAJI WA WATEJA JUU YA USAFIRI WA TRENI YA ABIRIA KUANZIA SIKU YA JUMATATU DESEMBA 16, 2019.

AWALI TRENI YA ABIRIA ILIKUWA IKIFANYA SAFARI KATI YA DAR ES SALAAM NA MOSHI TANGU TAREHE 6.12.2019 MARA NNE KWA WIKI, AMBAPO ILIKUWA IKITOKA DAR ES SALAAM SIKU YA JUMANNE NA IJUMAA, NA KUTOKA MOSHI SIKU YA JUMAMOSI NA JUMATANO. SHIRIKA LIMEFANYIA KAZI MAOMBI YA WATEJA KWA KUONGEZA IDADI YA SAFARI ZA TRENI KUWA MARA SITA KWA WIKI.

TRENI YA ABIRIA ITAKUA IKIANZA SAFARI KUTOKA DAR ES SALAAM KWENDA MOSHI SIKU ZA JUMATATU, JUMATANO NA IJUMAA SAA 10:30 ALASIRI NA KUTOKA MOSHI KUELEKEA DAR ES SALAAM SIKU ZA JUMANNE, ALHAMISI, NA JUMAMOSI SAA 10:30 ALASIRI.